Thursday, July 4, 2013

BILA SHAKA NI ALNOD TARIMO NDIO CHAGUO LA WANAUSHIRIKA


HII NI BAADA YA KUFUTWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI ULIOFANYIKA TAREHE 26/06/2013 SASA MCHAKATO UMEANZA UPYA NA MAJINA MAWILI YA WAGOMBEA YAKIWA TAYARI YAMETOLEWA NA TUME YA UCHAGUZI AMBAYO NI MOLLE NA ALNOD TARIMO NA KAMPENI ZIMEANZA. NA UCHAGUZI NI KESHO IJUMAA TAREHE 05/07/2013.

MATOKEO YA UCHAGUZI ULIOPITA YALIFUTWA KUTOKANA NA TUME WALICHOTANGAZA KUWA NI KUSHINDWA KUFIKIA ASILIMIA SABINI NA TANO YA WAPIGA KURA WALIOTARAJIWA. KITENDO AMBACHO WENGI WETU KIMESHINDWA KUINGIA AKILINI. KWANI HIYO ASILIMIA SABINI NA TANO INAYOTAKIWA NI VIGUMU SANA KUFIKIA LABDA KAMA WANA SABABU NYINGINE AMBAZO KIMSINGI HAZIKUZUNGUZWA HADHARANI KATIKA MCHAKATO WA KUIMARISHA DEMOKRASIA.

KATIKA UCHAGUZI ULIOPITA FIDELIS ZACHARIA NDIYE ALIYEKUWA MSHINDI LAKINI KWA BAHATI MBAYA AWAMU YA PILI HAKUWEZA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA TENA BAADA YA MCHAKATO WA UCHAGUZI HUO KUTANGAZWA KURUDIWA.

SASA TUNA SURA MPYA MOJA AMBAYO NI MTU MZURI ZAIDI YA FIDELIS ZACHARIA BWANA ALNOD TARIMO AMBAYE ALIKUWA SPIKA WA BUNGE WA SERIKALI INAYOONDOKA MADARAKANI (2012/2013).

NI KIJANA MWENYE SIFA NZURI KATIKA UONGOZI WAKE KWANI ALIONGOZA BUNGE KWA UADILIFU MKUBWA KIASI CHA KULETA CHACHU KATIKA SERIKALI INAYOONDOKA MADARAKANI.

NI MTU AMBAYE ALIKUWA HAFAHAMIKI MACHONI KWA WATU WENGI HAPA USHIRIKA LAKINI NI KIJANA AMBAYE ANA UWEZO MKUBWA KATIKA UONGOZI

SASA NDIYE MTU ANAYETAZAMIWA NA WENGI KUWA NDIYE RAISI MTARAJIWA WA MUCSO, AMBAYE ATALETA MABADILIKO KATIKA SERIKALI HIYO, BAADA YA CHAGUO LA WENGI BWANA FIDELIS ZACHARIA KUTOKURUDI TENA KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI KWA AWAMU YA PILI, SABABU AMBAZO MPAKA SASA HAZIJAWEKWA WAZI.

LAKINI BILA SHAKA MTU MZURI ZAIDI YA FIDELISI ZACHARIA TUMEMPATA NI
ALNOD TARIMON (BA-ME II) AKIWA NA MGOMBEA MWENZA WAKA BWANA GODFREY AMINADABU (DCMA I)

VOTE FOR ALNOD TARIMO!!!

No comments:

Post a Comment